Ndoa ni jambo la baraka ambalo hufanyika kwa muunganiko wa watu wawili yaani mume na mke kuamua kuishi pamoja kwa maisha yao yote mpaka kifo kiwatenganishe. KWANINI UNADHANI UNATAKA KUOA? 1; Umri umekwenda? 2;Upweke umekuzidi? 3;Unatafuta wa kukupikia,kukufulia na kusafisha nyumba? 4;Unataka kutuliza hamu yako ya ngono kila utakapojisikia? 5;Unataka kuanzisha familia na kupata watoto? 6;Rafiki zako wote wameoa hivyo na we huna budi? HAYA NI MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUAMUA KUOA AU KUOLEWA. I)Hakikisha unamfahamu mpenzi wako au mchumba wako vizuri na historia yake vzuri na hata familia yake na kujiridhisha kwamba anakufaa angalau hata miezi sita ili usije jutia baadae (II)Hakikisha hali yako kiuchumi ni nzuri na kwamba unaweza kumudu majukumu yote ya kifamilia yatakayojitokeza kama vile chakula,matibabu,ada za watoto nk. (III)Washirikishe ndugu zako wa karibu na hata marafiki zako kadhaa kuhusu kutaka kuingia kwenye maisha ya ndoa na chuja kwa makini ushauri wao na pia hapa usimsahau Mungu na hata viongozi wa kiroho

Post a Comment

 
Top