KANUNI YA TOZO LA PAPO KWA HAPO Kanuni hii ni ya sheria ya usalama barabarani sura ya 168 kama ilivyorejewa mwaka 2002, kifungu cha 95iliyotiwa sahihi na Waziri wa Mambo ya Ndani na kupewa namba30/2015 na kisha kutangazwa na Gazeti la serikali tarehe 30/01/2015. kanuni hii itatumika kulipisha faini papo kwa hapo kwa njia ya mtandao. Dereva akikutwa na kosa, askari ataingiza kwenye mashine maalumu namba ya usajili wa gari,nambari ya leseni ya gari,eneo lilipofanykia kosa,kosa lilipofanyikia kosa na kisha askari atatoa tiketi na kumpa dereva. tiketi hiyo pamoja na kuwa na namba kumbukumbu ya malipo pia itakua na maelekezo ya kulipa. Malipo hayo huweza kulipiwa kwa tigo pesa,M-Pesa,Airtel Money,Max Malipo aukupitia kadi yako ya benki(ATM za NMB na UMOJA SWITCH) na unatakiwa kulipa ndani ya siku saba. KANUNI YA KUWEKA NUKTA KATIKA LESENI ZA UDEREVA Kanuni hii itatumika sambamba na tozo ya papo kwa hapo. Hii itatumika kama ilivyoainishwa na kurejewa na kifungu cha 25A na 114A. Mfumo huu sasa utahuisha uwekaji wa nukta kwenye leseni kutokana na uzito wa kosa. Mfano,kutokufunga mkanda ni nukta moja,uendeshaji wa hatari nukta tatu,na mwendokasi nukta tano na mara zifikapo nukta kumi na tano basi dereva ataufungiwa leseni kwa miezi sita. TUWE MAKINI

Post a Comment

 
Top