Papai ni miongoni mwa matunda yanayopatikana katika majira yote ya mwaka lakini ni wachache wanaofahamu kwamba lina manufaa zaidi ya kuliwa au kutengenezwa juisi. Faida zake ni pamoja ni kuwa hutunza ngozi na nywele maana ndani yake huwa na vitamini A ambayo huondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kuifanya ngozi kuwa kavu na hivyo kuondoa uwezekano wa kupata chunusi. Papai na asali husaidia kuondoa mikwaruzo na mikunjo inayoweza kujitokeza usoni. Papai pia linasaidia kwenye matunzo ya nywele. Sambamba na hilo,mbegu za papai zilizosagwa kwa kuchanganywa na mtindi hutumika kama tiba ya mba na ngozi kavu ya kichwa

Post a Comment

 
Top