Maandamano ya chama cha CHADEMA yaliyokua yanafanyika huko Mwanza yamegeuka vurugu baada ya wandamanaji kuanza kupambana na polisi. CHADEMA walikuwa wakiandamana katika kushinikiza Meya wa Ilemela Henry Matata aachie ngazi kwani hana sifa zakua meya, baada ya kuvuliwa uanachama na chama hicho. Katika picha zilizokirushwa kupitia televisheni ya Barmedas Tv ya Mwanza, barabara zimeonekana zikiwa zimefungwa kwa mawe na miti, huku katika maeneo mengine uchafu ukiwa umejazwa barabarani na matairi kuchomwa. Katika mtaa wa Mission waandamanaji wamefunga barabara kwa uchafu uliokua katika dampo moja kando ya barabara hiyo. Maandamano hayo yalikuwa yamalizikie viwanja vya Furahisha ambapo viongozi wa CHADEMA walitarajiwa kuhutubia. -

21 Aug 2015

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top