http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/08/3X6A4031.jpg
Leo katika viwanja vya Jangwani CCM imezindua kampeni zake rasmi na kuhudhuriwa na viongozi wastaafu na makada wengi wa chama hicho mahiri katika siasa za hapa Tanzania.
Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi katika uzinduzi wa kampeni za CCM leo katika viwanja vya jangwani palikuwa hapatoshi kwa mafuriko ya wana CCM walijitokeza kwa maelfu kushuhudia uzinduzi huo.
3X6A4035
3X6A3978
Hongereni sana CCM mmeanza vizuri sana kwa kuonesha kuwa mpo imara bado pamoja na mpalaganyiko wa hapa na pale uliopelekea baadhi ya makada mahiri kutimkia upande wa pili.Watanzania wengi bado wanaimani na CCM katika kusukuma gurudumu la maendeleo na kutuvusha pale tulipokwamia.Wananchi wengi wameonesha imani kubwa kwa Mh. John P. Magufuri na ni imani ya wengi kuwa atafanya kitu cha tofauti pindi atakapopewa ridhaa ya wananchi ya kwenda pale Magogoni ili aweze kuwatumikia.

Ingawa kwenye uzinduzi wa leo nilitaka kuingiwa na shaka kidogo pale nilipoona jukwaa linataka kugeuka kuwa jukwaa la mipasho kwa wale mahasimu wenu kisiasa badala ya kutoa na kufafanunua sera ambazo ndio kiu kubwa ya Watanzania wengi.
3X6A4036
3X6A4071

Post a Comment

 
Top