TAHARUKI UKAWA, SUMAYE KUOKOA JAHAZI
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye mchana huu AMEJIUNGA na
Chama Cha NCCR-Mageuzi katika kile kinachoitwa "Mpango Mbadala"
kutokana na imani ya viongozi wa UKAWA kwamba lolote litatokea kwa Mgombea
wa UKAWA kutokana na hali yake ya afya kuendelea kutetereka kwa kasi.
Mazungumzo kati ya UKAWA na Bwana Sumaye yamechukua uharaka mpya hivi
karibuni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi hiki kifupi ambacho
viongozi wa UKAWA wamekuwa karibu na Bwana Lowassa ndipo wameshuhudia
ukubwa wa tatizo lake la afya na katika vikao ambavyo havikumhusisha
Lowassa wamejiridhisha kwamba hataweza kufanya kampeni nchi nzima kwa
ufanisi na kwamba, hata kama wakishinda uchaguzi, Bwana Lowassa hatakuwa
na uwezo wa kuendesha Serikali.
Aliyeongoza mazungumzo ya kumshawishi Bwana Sumaye ni Bwana James
Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, Askofu Sendoro wa KKKT, Mchungaji
Mtaita. Askofu Stephen Munga wa KKKT pia alihusika kwa nyakati tofauti.
Bwana Sumaye, ambaye amekuwa hasimu mkubwa wa Bwana Lowassa,
alishawishiwa kwa hoja tano:
Viongozi wa UKAWA walimshawishi Bwana Sumaye kwamba wana nafasi ya
kushinda lakini wana uhakika kwamba Bwana Lowassa hatakuwa na nguvu,
afya na uwezo wa kuendesha Serikali kwahiyo yeye, kwa utaratibu mahsusi,
ndiye atakayeendesha Serikali. Lakini pia walimshawishi kwamba
litakapotokea lolote kwa Bwana Lowassa yeye ndio atakuwa Mgombea wa
UKAWA.
Pia Bwana Sumaye alishawishiwa kwamba maisha yake yatatazamwa na
hatakuwa na matatizo tena ya kifedha. Aliyechukua jukumu la kumlipa
Bwana Sumaye kwasasa na baadaye kumtengenezea uchumi ni Bwana Anselm
Minja, Mfanyabiashara wa Arusha.
Baada ya kuijulisha familia yake, taharuki imezuka huku familia nzima
ikipinga suala hili la kuhamia UKAWA. Familia ya Sumaye ilikuwa na hoja
tatu,
Kwanza: heshima ya Sumaye, ambaye sifa yake kubwa ni msimamo, itashuka
kutokana na ukweli kwamba kwa miaka yote amekuwa akimsema Lowassa kwamba
ni fisadi na aliwahi kutamka kwamba Lowassa akipitishwa na CCM yeye
anaenda UKAWA. Sasa leo yeye ndiye anamfuata Lowassa alipo kwasababu ya
madaraka.
Hoja ya pili ya familia ni hofu ya kitakachotokea pale UKAWA
itakaposhindwa uchaguzi. Familia inakumbuka jinsi Sumaye alivyoporomoka
kisiasa mara baada ya kushindwa mwaka 2005 na inakumbuka zaidi jinsi
alivyodhalilika baada ya kushindwa kwenye U-NEC wa CCM na Mary Nagu
kwamba 2012.
Familia inaamini kwamba wakati wa Sumaye kisiasa nchini umeshapita na
Kwa kujiingiza kwake kwenye upinzani anaharibia wanae ambao wana maisha
mbele zaidi.
Post a Comment