Aliyekua Mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila, anatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee na kisha kusafirishwa kwa ajili ya mazishi nyumbani kwao Ludewa. Mchungaji Mtikila alifariki jumapili alfajiri baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Chalinze wakati akitokea Njombe kwenye kampeni. Atakumbukwa kwa kuwa mmoja wa wapigania haki hasa kwenye masuala kama ya kuidai Tanganyika na suala la mgombea binafsi. Mungu ailaze roho ya marehem mahala pema peponi, amin.

Post a Comment

 
Top